Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Watu wa China kupitia Ubalozi mdogo wa China uliopo Zanzibar, China imesema inatarajia kuipatia Serikali ya Zanzibar $100,000,000 sawa na Tsh: 34.9Billion. kwa mwaka huu 2018 ruzuku hiyo itaelekezwa katika kusaidia sekta ya Uvuvi, Ushirikiano wa kiufundi wa kituo cha Radio, Ujenzi wa nyumba za Madaktari, Ujenzi wa taaa za barabarani, uchimbaji wa visima kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar pamoja na kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na ya muda mfupi watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Uwekaji wa Sain hiyo umetiwa na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Khalid Salum na Balozi mdogo wa China mjini Zanzibar. tarehe 16/01/2018.

 
Katika kuimarisha Uekezaji nchini ( Foreign Direct Investment), Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ameweka jiwe la msingi la mji mpya wa nyumba za maendeleo (Zanzibar Fumba Town Developmennt) uliopo katika vijiji vya Nyamanzi Dimani. Nyumba hizo za masharti na mkopo nafuu zinamazingira mazuri na Miundombinu ya hali ya juu, Uwekezaji huo umelenga kusaidia dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwapatia wananchi wake makaazi bora. Mhe. Rais aliwataka wanamchi kuitumia kikamilifu fursa hiyo ambayo inaendana na malengo ya Taifa ya kukuza Uchumi na kupunguza umaskini kufikia kiwango cha kati ifikapo mwaka 2020.uwekaji jiwe hilo la msingi ulifanyika tarehe 11/01/2018.

Zanzibar